Date: 19 – 21 August 2026
Time: 3:00 Asubuhi – 11:00 Jioni (9:00 AM – 5:00 PM)
Location: Mwanza Women’s Hospital, Rufiji Street, Mwanza, Tanzania
Lengo Kuu la Kambi
Mwanza Women’s Hospital inawaletea Kambi ya Uchunguzi na Matibabu ya Matatizo ya Uzazi kuanzia tarehe 19 hadi 21 Agosti 2026. Lengo kuu la kambi hii ni kutambua na kuwahudumia wagonjwa wanaokabiliwa na changamoto za uzazi ambao wataweza kunufaika na matibabu bobezi ya uzazi, ikiwemo upandikizaji wa mbegu na mayai (IVF).
Huduma hizi zote zitatolewa kwa gharama nafuu maalum wakati wa siku hizi tatu za kambi.
Watakaokuhudumia (Visiting Specialists)
Katika kambi hii, utapata fursa ya kufanyiwa uchunguzi na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari mabingwa waliobobea katika masuala ya uzazi kutoka nchini India na Tanzania:
- Dr. Tarun Javali Dilip – Urologist / Andrologist (India)(Mbingwa wa Mfumo wa Mkojo na Uzazi wa Kiume)
- Dr. Chaitra Narayan Nayak – Fertility Specialist (India)(Mbingwa wa Afya ya Uzazi na Upandikizaji)
- Dr. Andrew Kilonzo – Obstetrician / Gynecologist (Tanzania)(Mbingwa wa Akina Mama na Uzazi)
Huduma Zitakazotolewa Katika Kambi
🚺 1. Uchunguzi wa Kina kwa Wanawake:
- Ultrasound: Uchunguzi wa kina wa mfumo wa uzazi wa mwanamke.
- Uchunguzi wa Mirija: Kuangalia kama mirija ya uzazi iko wazi au imeziba.
- Vipimo vya Homoni: Kupima kiwango cha homoni zinazohusika na upevu wa mayai.
- Upasuaji wa Matundu (Laparoscopy): Uchunguzi na matibabu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya matundu madogo.
🚹 2. Uchunguzi wa Kina kwa Wanaume:
- Uchunguzi wa Mbegu (Semen Analysis): Uchunguzi wa kina wa afya ya mbegu za kiume (idadi, umbo, na mwendo).
- Vipimo vya Homoni: Kupima homoni zinazochochea uzalishaji wa mbegu.
- Ultrasound: Uchunguzi wa viungo vya uzazi vya kiume.
🧬 3. Maandalizi ya Matibabu ya Upandikizaji (IVF):
Kwa wanandoa wanaohitaji huduma za upandikizaji (In Vitro Fertilization – IVF), madaktari wetu mabingwa watafanya uchunguzi wa kina wa awali pamoja na kuweka mipango na maandalizi kamili ya matibabu hayo mapya na ya kisasa.
📞 Wahi Kufanya Appointment Mapema!
Nafasi ni chache na huduma zitakua kwa miadi tu. Wasiliana nasi sasa ili kuhifadhi nafasi yako:
- 📱 Simu / WhatsApp: +255 754 666 484
- 📍 Mahali: Mwanza Women’s Hospital, Rufiji Street, Mwanza, Tanzania






